BREAKING NEWS

Habari

Mkesha wa mwaka mpya

Tangaza nuru juu ya mwaka 2016

Nabii jiographia

Tangaza Nuru katika maisha yako

Shuhuda

Matangazo

Mahubiri

Wednesday, January 20, 2016

Ujumbe: Mashaka ya Nabii Musa!

Ujumbe: Mashaka ya Nabii Musa!
Kutoka 3:1-4:17
1. Mungu alipomtokea Musa katika kijiti kilichokuwa na utukufu
a. Alimuita Musa ili kuwaongoza Israel kutoka katika Inchi ya Utumwa Misri
b. Musa alionyesha Mashaka Yake wazi na kutoa sababu zinazodhihirisha kwa nini hafai kwa Kazi hiyo
2. Musa alionyesha Mashaka yake wazi na Bwana Mungu alikuwa akimjibu Musa, Msahaka ya Musa ndio somo kubwa sana kwetu
a. Kwa sababu ni katika nia inayofanana watu wengi sana leo hupewa na Mungu wajibu Fulani na hata wito wa kumtumikia Mungu
b. Si kwaajili ya kuwatoa watu katika utumwa kama ilivyo kwa Musa kule Misri, lakini kwa Ulimwengu kwaajili ya kuwahubiri habari njema Marko 16:15 1Petro 2:9 ili waokolewe
c. Kama ilivyokuwa kwa Musa wengi wetu tunatoa Udhuru na kuonyesha Mashaka, Mashaka ya Musa yanaweza kugawanywa katika maeneo Matano yafuatayo
A. Mimi ni nani? Kutoka 3:11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani……
1. Ingawa Musa aliwahi kuishi katika Ikulu ya Farao mtawala wa Misri
a. Sasa alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwewe akiwa mtu duni
b. Miaka 40 ilikuwa imepita tangu alipoondoka kwa Farao
c. Sasa alikuwa mtu mzima mzee wa miaka 80, nguvu za ujana zimekwisha na yuiko na fimbo tu Musa aliweza kuwa na sababu za haki za kufikiri kuwa huenda yyeye si mtu sahii
2. Mungu alimjibu Musa Kutoka 3:12 asiwe na Mashaka kwani yeye atakuwa Pamoja naye
a. Bila shaka mimi nitakuwa Pamoja nawe
b. Mungu anapomuahidi mtu atakuwa Pamoja naye maana yake Yeye mwenyewe Mungu ni Utoshelevu wetu
c. Paulo mtume alisema kama Mungu akiwa Upande wetu yaani pamoja nasi ni nani atakayeweza kusimama kinyumenasi Warumi 8:31
B. Baadhi yetu leo tunatoa Udhuru au kuonyesha Mashaka kama Musa
1. Tunajiangalia wenyewe na kujipima na kuona kwamba hatutoshelezi/hatustahili kwa vigezo vya kuwa watumishi wa Mungu
a. Ni kweli kabisa hakuna mwanadamu anayetosheleza katika utumishi na huduma hii kimsingi hata mimi pamoja na kujiita Mkuu wa wajenzi katika Huduma hii kila siku najigundua kuwa sistahili kabisa kumtumikia Mungu, sio hivyo tu huwa namshangaa Mungu kwa nini anitumia mtu kama mie
b. Lakini Mungu ni Utoshelevu wetu 2Wakoritho 3:5-6 “ Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu, Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya”
c. Unaudhuru gani Elimu? Angalia kuwa Mungu aliwatumia mitume ambao wengi wao walikuwa wasio na Elimu Matendo 4:13
d. Kama ilivyokuwa Mungu kwa Musa, Yesu Kristo anakutia moyo leo usiogope atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari Mathayo 28:20
e. Kwa msaada wake tutayaweza yote Wafilipi 4:13.
C. Niwaambie Nini? Imekaa vema kwa kimombo what shall I say? Kutoka 3:13
1. Musa alijua kwamba anapaswa kuwaendea Israel, na wako kifungoni wakiwa na maswali lukuki
a. Wangemuuliza Mungu yupi aliye kutuma?
b. Kwa nini tuondoke hapa tumekuweko kwa miaka 400, tumezaliwa hapa haya ndio maisha yetu na tamaduni zetu
c. Ni kama Musa alukuwa akijiuliza ninaanzia wapi?
2. Mungu alilazimika tena kumjibu Musa, mwenye mashaka
a. Mimi niko ambaye niko, Utawaambia Kutoka 3:14-15
b. Mungu alikuwa na majibu kwa Musa kuhusu nini cha kusema
D. Baadhi yetu tunaweza kuwa na mashaka kuhusu nini cha kusema
1. Tuna mashaka kwa sababu wakati mwingine tunafikiri kuhusu maarifa yetu yasotosheleza
2. Lakini Mungu ataweka maarifa na nini cha kusema
a. Atakupa neno rahisi Marko 16:15-16
b. Na ni jinsi gani itakuwa Rahisi 1Koritho 15:1-4,2:2
c. Hata Musa alipokuwa ameelekezwa nini cha kusema akaibuka na sababu nyingine
E. Je wasiponiamini wala kunisikiliza?
1. Musa sasa amepewa Maarifa na anajua nini cha Kusema lakini anawasiwasi hawatamuamini walakumsikiliza?
a. Ni dhahiri kuwa Musa alikuwa anaogopa kukosea
b. Anaogopa matokeo magumu na amesahau kuwa Mungu alisema atakuwa Pamoja naye
2. Mungu alimsaidia Musa kuondoa mashaka na kumuaminisha kuwa yuko naye
a. Fimbo ya Musa iligeuka kuwa nyoka Kutoka 4:2-5
b. Mkono wake ulipatwa na ukoma
c. Maji yaliyogeuka Damu Kutoka 4:9.
F. Wengi wetu tunamashaka na majukumu na wajibu tuliopewa kuutumikia na kwa watu wa Mungu wana mashaka kama wanafaa kuwa chombo cha kuhubiri injili
1. kumbuka woga ni adui anayekuzuia katika kujaribu
2. Kama Mungu alivyomjibu Musa na kuondoa mashaka aliyokuwa nayo tunao ushahidi unaoweza kututhibitishia na kutuondolea mashaka juu ya kile Mungu anataka tukitimize
a. Neno la Mungu liko kwaajili yetu Warumi 10:17, Yohana 20:30-31
b. Yesu alikufa na maefufuka Yuko hai ni yeye anayetenda kazi ndani yetu
c. Migandamizo na kelele kutoka nje isikutie mashaka ukaacha kumuamini Mungu kuwa yu aweza kukusaidia na kuwa yuko pamoja nawe na kuwa vita si yako ni yake yeye na kuwa hata wajibu na kazi tuliyopewa ni kwa utukufu wake.
G. Mimi sio Msemaji, Mimi sio mwepesi wa Kusema!
1. Tunaona mashaka haya katika Kutoka 4:10
1. Musa alisema mimi sio mnenaji Mzuri? Je umeshawahi kuwasikia baadhi ya viongozi wakisema neno mimi sio Mwanasiasa? Unajua wanamaanisha nini? Wao sio wasemaji, sio wazungumzaji wazuri
2. Mungu hasukumwi na Udhaifu wa Mwanadamu anatujua tulivyo hata kabla hajakuita au kukupa wajibu
3. Anaujuzi wa kuwatumia hata waliodhaifu ndio si tuliumbwa kwa kusudi lake uwe na uwezo usiwe na uwezo yeye akiamua anakutumia
a. Mungu alimsaidia Musa kujua Yeye ndiye Muumba ndiye anayeruhusu mtu kuwa Bubu au kuwa msemaji, Mungu alikuwa anaelewa wazi udhaifu wake na kama udhaifu wake ungekuwa ni sababu ya yeye kushindwa kumtumia asingelimfuata
b. Mungu anauwezo wa kumsaidia kila mtu katika madhaifu yake
c. Mungu alimuahidi tena Musa kuwa atakuwa pamoja naye Kutoka 4:11
d. Mungu alimuandaa haruni kwaajili ya kumsaidia Musa Kutoka 4:14-16 Mungu wakati wote ataandaa watu wa kututia moyo na kufanya kazi pamoja nasi.
H. Sisi nasi tunaweza kuwa na mashaka na kutoa udhuru kama huu wa Musa,
1. Paulo mtume Hakuwa na ufasaha wa Maneno wala hekima kama zile za wagiriki, alikuwa dhaifu, mwenye hofu na mwenye kutetemeka sana 1Koritho 2:1-5, Lakini pamoja na hayo alimtegemea Mungu na sio hilo tu aliwatia moyo na wengine
“Imani yetu isiwe katika Hekima za wanadamu bali katika nguvu za Mungu”
Musa aliogopa kuwa mnenaji eti kwa vile alikuwa na Kigugumizi Kutoka 4:13 Mungu hakukiondoa kigugumizi kila japo angeweza kufanya hivyo Mungu alikusudia kumtumia pamoja na udhaifu wake
I. Tuma huyo utakayemtuma! Kutoka 4:13.
Mungu alikubaliana na Mashaka yote ya Musa na kila mashaka yake yalikuwa na Majibu lakini sasa Mungu anakasirishwa na tabia ya Musa wakati huu, Sasa Musa hataki kabisa kwenda!
1. Mungu ametuumba kwa kusudi lake ni lazima tutmika bila kujali udhaifu tulionao kwa vila kila aina ya udhaifu una majibu kwa Mungu
2. Ukikataa kumtumikia Mungu au kulitumikia kusudi la Mungu unajiweka katika wajibu wa kumtumikia shetani
3. Hasira za Mungu kwa Musa zilikuwa za upendo, Mungu alikuwa anataka kumtumia Musa ndiye aliyekuwa amamemuandaa kwa Muda mrefu kwa kusudi hilo
Ndugu zangu
a. Kila udhuru na kila sababu utakayoitoa kukwepa kutokumtumikia Mungu ni Upotoshaji wa haki ya Mungu
b. Ni kweli tungetamani kama Mungu angelimtumia mtu mwingine mbadala
c. Ni kweli hatupendi kutenda kila Mungu anachokitaka
d. Lakini ndugu hapo ndipo hasira za Bwana zinapowaka na kuwa kinyume nasi, hatuwezi kuacha kulitumikia kusudila Mungu wetu hata kama kuna hali zinazokataa endapo hali hizi zimetokea kwetu kutoa udhuru tunahitaji kutubu
Hatimaye!
Wote tunajua kuwa Musa alikubali, wito wa kwenda Misri
Wote tunajua kuwa Mungu alikuwa pamoja naye na kumsaidia
Wote tunajua dhahiri kuwa Musa sasa anaheshimika na kukubalika na watu wote kama kiongozi mkubwa sana wa manabii na baba wa taifa la Israel, Ukiondoa shaka na kumuamini Mungu atakutumia kwa viwango vya juu kwa utukufu wake.
Mungu hatuimii watu maalumu sana, Tunakuwamaalumu Mungu anapokuwa Pamoja nasi
God never use the superman, we became the superman when God is with us


Innocent Kamote's photo.
IMECHAPISHWA NA REV:INNOCENT KAMOTE

Tuesday, January 12, 2016

KAMA SI BWANA ISRAEL NA ASEME SASA


KAMA SI BWANA ISRAEL NA ASEME SASA

Muhubiri; Mchungaji Innocent kamote

Zaburi ya 124;1-8.

     Zaburi ni mojawapo ya vitabui vya kipekee sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano, inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana  na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa hisia za watu

·    Zaburi zilia ndikwa kwa sababu mbalimbali za kihisia kam avile watu walipokuwa na furaha ,huzuni,nk, Mfano mwandishi wa wimbo nionapo amani kamqa shwari kwa hiyo kuna sababu nyingi zilizopelekea zaburi kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na

1.      Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili mfano zaburi ya 1

2.      Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingu huanza kwa kusema mshukuruni Bwana

3.      Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27

4.      Zaburi za kifalme au za kimasihi

5.      Zaburi za kihistoria au za kukumbuka matukio maalumu

6.      Zaburi za kusifu au Halel Psalms ambazo huanza na neno Haleluya

7.      Zaburi za maombolezo

8.      Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani Mfano Zaburi ya 35 : 1-8

Zaburi ya 124 ni zaburi ya kihistoria ni ya kukumbuka matukio na ni zaburi inayokisiwa kuwa ya Daudi au mtu wa karibu na Daudi Kwani Zaburi zimeandikwa na watu wengi akiwemo Musa, Sulemani wana wa kora n.k na Daudi anazo zaburi kama 73 hivi na nyingine ni zaburi yatima  Zaburi hii ya 124 inakisiwa ndiyo iliyonukuliwa na Paulo katika Warumi 8;31 “Mungu akiwa upande wetu ni nani atakayekuwa juu yetu?” Inaonekana mwandishi wa zaburi hii alikuwa akitafakari kwa niaba yake na kwaniaba ya Taifa la Israel  jinsi hasira za adui shetani zilivyokuwa juu yao jinsi alivyokusudia kuiangamiza Israel kwa moto, maji, mitego na mbinu mablimbali, jinsi alivyokusudia kutumaliza lakini hatimaye anaanza na hitimisho kuwa kama Bwana asingelikuwa pamoja nasi Tungeliangamia huku Israel wakiwa mashahidi ya wema wa Bwana na utetezi wa Mungu Hivyo kama si bwana Israel na aseme sasa

Israel ni taifa linalotetewa na Mungu hata leo ni mara kadhaa wamepitia  misukosuko ambayo isingelikuwa rahisi kuiepuka kwa hali ya kawaida, wakristo wengi wasio na ufahamu hufikiri kuwa kanisa ni mbadala wa Israel, Warumi 11:1-2 Israel ni kijiti kinachowaka moto lakini hakiteketei!

*                   1948 – wayahudi walipopata uhuru wakiwa kiasi cha wayahudi laki sita hivi kuhesabu wanawake na watoto Waarabu wakiwa miliono 80 walikusudia kuwa futilia mbali lakini kwa uweza wa ajabu Israel Iliwapiga vibaya wqaarabu na kufanikiwa kupanua mipaka yao kutoka Tell Avivi Jaffa mpaja ukanda wa gaza, milima ya Golan, na kuuteka mji wa Yerusalem

*                   1950 – Wafaransa walikuwa ndio wafadhili wakubwa wa kuuza ndege za kivita kwa Israel lakini katika vita ya Six days War Israel walionyesha kipigo kikali sana kwa maadui ambacho wafaransa walisema kipigo hicho hakiwezi kusababishwa na ndege zao kwa hivyo uhusiano na Isarael kijeshi ulisimama kwani Israel walikuwa wakiziboresha ndege hizo na zikatoa kichapo kikali

*                   June 5 1967 – Isarel kwa dakika 3 tu walizipiga ndege za maadui 451 zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuifuta Israel ndege hizo mpya zilizonunuliwa na wamisri na nyingine za Jordani na Syria  zilitandikwa vibaya na hivyo kupelekea Misri na Jordani kuweka mkataba wa kudumu wa amani na Isarael kuwa hawatapigana tena milele

*                   1969-1970 – Ndege 111 za maadui ziliwekwa chini pamoja na msaada wa warusi katika vita hiyo waarabu waliaibiika

*                   Jeshi la anga la Israel limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na katika operation mbalimbali waliweza kuwalenga viongozi wa kigaidi wa palestina kwa vipimo vilivyoweza kuwapata na kuwaua mmoja mmoja viongozi hao ni pamoja na Abu ali Mustafa, Ahmed Yasini na Abed al azizi Rant iss aliyeuawa punde akitokea msikitini wakati wa ibada ya ijumaa

*                   1976 walifanikiwa kuokoa  wayahudi kadhaa waliokuwa wakitishiwa kuuawa na Iddi amini dikteta aliyetawala Uganda katika operation iliyoitwa operation Entebe

*                   1991 – Jeshi la anga la Israel lilifanikiwa kuwaokoa wayahudi wenye asili ya kiafrika huko Ethiopia wanaoshukiwa kuwa ni watoto wa mfalme suleimani  Katika operation iliyoitwa operation Solomon

Sisi nasi tunapotafakari maswala ambayo adui ameyakusudia kwetu na kuona ushindi wa ajabu ni muhimu kufahamu kuwa kama si Mungu kuwa upande wetu tungelifutiliwa mbali kweli Kama si Bwana Israel na aseme sasa!

 

Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu?

Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Luka 6: 39
Ndugu msomaji wangu imani yangu ni kuwa kama macho yako yameongozwa kusoma habari hii basi bila shaka Roho wa Mungu anataka utafakari pamoja nami kuhusu aya hiyo hapo juu leo.
Tunapotafakari kuhusu mstari huo ni mithali iliyotolewa na Bwana Yesu juu ya kanuni fulani ya uongozi Kutokana na andiko hilo ni wazi Yesu anamaanisha ili mabadiliko yatokee ni wazi kuwa kiongozi anapaswa awe na maono au mtazamo tofauti na wale anaowaongoza ndipo badiliko linaweza kutokea Kama kiongozi ana maono na mtazamo uleule walionao watu wake hakuna badiliko laweza kutokea JE KIPOFU AWEZA

 

Monday, January 4, 2016

HAKUNA NGUVU YA MAPEPO WALA WA CHAWI INAYO WEZA KUDUMU


Habari ndugu mpendwa msomaji wa nakara zangu.siku hii ya leo ninayo habari njema kwako ya kwamba akuna nguvu za giza ama nguvu za kichawi zaniazo dumu.sizani kama wanielewa sawa sawa,Nguvu za giza siku zote zime tengenezwa kwa ajiri ya giza na ndio maana mwanga unapo ingia katika giza giza hutoweka maramoja.ivyo siku zote hakuna nguvu ya wachawi inayo dumu bali kinacho dumu ni nguvu ya Mungu tu.kama upo na biblia yako karibu unaeza fungua nami ISAYA 54:1-4 isaya anatupa unabii ya kwamba maisha yetu yote yamewekwa kiganjani pake Mungu ivyo tusiogope wala tusifadhaike.panua mahari pa hema yako na uyatandaze maskani yako ongeza urefu wa kamba zako katika bihashara yako,elimu yako,maono yako,familia yako nauone ni jinsi gani Mungu atakavyokwenda kukubaliki.kwani Mungu kupitia Nabii wake isaya anatuahidi yakuwa (angaria mstari wa 3),kwa maana utaenea upande wa kushoto;na wazao wako watamiliki mataifa;wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa nawatu. nasema kama Nabii ya kwamba biashara yako ikaongezeke kwanzia sasa katika jina la Yesu,wewe mfanyakazi Mungu akakufugulie milango katika jina la Yesu, Ahadi zako ambazo Mungu amepanga kwa ajiri yako ukapoke katika jina la Yesu.Wachawi wanaweza wakaharibu maisha yako lakini shika hii HAKUNA NGUVU YA WACHAWI AU MAPEPO INAYOWEZA KUDUMU.Nguvu ya Mungu ndio nguvu pekee inayo weza ikadumu milele.mathayo24:35 biblia inatueleza kuwa mbingu na nchii zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe na ndio maana wachawi awata fanya uchawi wao bila siku moja kukamatika adharani kwani atujakamata wachawi hapa? bonyeza link hii upate soma nakara hii iliyo pita kuhusu wachawi.Ninaamuru nguvu yakushinda wachawi ikufuate katika jina la Yesu ukapate kuwajua wa baya wako wote na uwajuapo tu usiwape nafasi kazi yako ni moja wewe tangaza nuru uone jinsi ambavyo mambo yako yataenda sawa.Ninapomalizia ninapenda kukushauri mwaka huu usipoteze muda kujadiri mambo yasio faa bari kaa chini kujadiri mambo yatakayo kuletea faida na sii hasara ubalikiwe sana!



FANYA MAMBO MPAKA WATU WASHANGAE.


Mpendwa mfatiliaji wa makara zangu nilizo kuwa nikiziandika kupitia blog yangu.leo nimekuletea ujumbe mpya ambao ukiamasika na ku ushika nakuufanyia kazi utakuinua sana.



Siku zote watu wamekuwa wakipoteza muda katika jumla ya maisha yao walio ishi kwani wamekuwa wakiishi kwa ajiri ya kumfurahisha mwanadamu,bila ya kuishi kwa ajiri ya Mungu,adi badae kujikuta kuishia bila mafanikio yoyote adi uzee wao wote.Biblia inatufundisha kupitia mfano wa yuda escarioti ambaye alikuwa amepewa cheo cha mtunza azina kati ya wanafunzi wa Yesu alifanya mambo yakeyote kwa ajiri ya kuwafurahisha wanadamu na mwisho kuishia patupu kwani wanadamu ao ao walioneka kuwa wabaya kwake adi badaye aliamua kwenda kujiua katika bonde la alkadema.Yesu anatueleza katika Mathayo13:18c "aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake" Neno hili lilikuwa limemlenga yuda kwani alikuwa ni mwanafunzi wa Yesu ambaye aliaminiwa kupita kiasi na Rabii wake,lakini kwa jambo alilolifanya yuda ambalo lilimgarimu sana adi kutoa uhai wake nikufanya mambo kwa ajiri ya wanadamu na sii kwa ajiri ya Mungu.Na ndio maana wakati ule wa chakula cha usiku Yesu alisema ya kwamba yeye aliyetia mkono wake katika kombe ili ndiye atakaye nisaliti nabaadae kwisha kumpatia tonge na kumlisha nakusema..... angaria mstari wa 26.sikuzote unapo fanya mambo yako kwa ajiri ya mwanadamu shetani anakuwa karibu nawe ili kukupoteza nandio maaana yuda aliingiwa nashetani npale tu ambapo  Yesu alikuewa amekwisha kumpatia tonge ndipo Yesu akamwambia "uyatendayo uyatende upesi" sikuzote Mungu anapoona umemueka mbali naye uwa anakuacha na Mungu akikuacha akuna kitakacho weza kuwezekana na ndio maana yuda akuchukua Muda akajijutia alicho fanya na akaamua kwenda kujiua katika bonde la alkadema ambapo uko aliweza kupoteza uhai wake sio uyo tu ila tuna mifano mingi katika Biblia sitatoa yote ila nitakueleza huu mmoja ambao utakufundisha.Fungua pamoja nami katika kitabu cha mwanzo 3 kaini alikuwa ni mmoja wamtu ambaye alikuwa mbali na Mungu kwani biblia inatueleza kuwa alipo jua amemtenda kosa bwana akukumbuka ata kuomba msamaha na ndio maana katika mstari wa  9:kaini akasema "mimi ni mlinzi wandugu yangu" hapa ni baada ya kuulizwa abel yukwapi biblia inatueleza Mungu alimlaani kaini ni kumuacha afate akili yake yakibinadamu na mwisho wakaini au kua mzuri      kwani Mungu alimuacha afanye mambo yake.unapo fanya mambo yako sikuzote usifanye kwa ajiri ya Mtu ila jitaidi kufanya mambo kwaajiri ya kumtukuza Mungu kwani mwanadamu atakusaidia chochote mwisho wamwanadamu nikukusemea mabaya tu.Miguu yako iwe moto ili kila yupitapo mbaya wako akapate kuona moto uo katika jina la Yesu pokea.

Saturday, January 2, 2016

JIONEE KATIKA PICHA









Friday, January 1, 2016

BAADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA 2016

Tarehe 3/1/2016 kutakuwa na ibada ya kwanza ya kinabii mwaka 2016.tunapenda kukukaribisha katika ibada hii itakayo kuwa imejaa unabii na ata nuru katika maisha yetu.kutakuwa na waimbaji kama vile mtumishi wa Mungu Suleiman,matumaini,na prays team ya reveration church of Tanzania.ibada hii itaongozwa na Nabii jiographia usionapo tangazo hili mfahamishe na mwenzio hakikisha unakuja na mtu mwingine.kuwai kwako ndio kupokea kwako Zaidi ameen.kwa mawasiliano Zaidi piga simu namba <strong>0656240305</strong>
 
Copyright © 2015 Nabii Jiographia

Designed by Luzmik Technologies