BREAKING NEWS

Monday, January 4, 2016

HAKUNA NGUVU YA MAPEPO WALA WA CHAWI INAYO WEZA KUDUMU


Habari ndugu mpendwa msomaji wa nakara zangu.siku hii ya leo ninayo habari njema kwako ya kwamba akuna nguvu za giza ama nguvu za kichawi zaniazo dumu.sizani kama wanielewa sawa sawa,Nguvu za giza siku zote zime tengenezwa kwa ajiri ya giza na ndio maana mwanga unapo ingia katika giza giza hutoweka maramoja.ivyo siku zote hakuna nguvu ya wachawi inayo dumu bali kinacho dumu ni nguvu ya Mungu tu.kama upo na biblia yako karibu unaeza fungua nami ISAYA 54:1-4 isaya anatupa unabii ya kwamba maisha yetu yote yamewekwa kiganjani pake Mungu ivyo tusiogope wala tusifadhaike.panua mahari pa hema yako na uyatandaze maskani yako ongeza urefu wa kamba zako katika bihashara yako,elimu yako,maono yako,familia yako nauone ni jinsi gani Mungu atakavyokwenda kukubaliki.kwani Mungu kupitia Nabii wake isaya anatuahidi yakuwa (angaria mstari wa 3),kwa maana utaenea upande wa kushoto;na wazao wako watamiliki mataifa;wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa nawatu. nasema kama Nabii ya kwamba biashara yako ikaongezeke kwanzia sasa katika jina la Yesu,wewe mfanyakazi Mungu akakufugulie milango katika jina la Yesu, Ahadi zako ambazo Mungu amepanga kwa ajiri yako ukapoke katika jina la Yesu.Wachawi wanaweza wakaharibu maisha yako lakini shika hii HAKUNA NGUVU YA WACHAWI AU MAPEPO INAYOWEZA KUDUMU.Nguvu ya Mungu ndio nguvu pekee inayo weza ikadumu milele.mathayo24:35 biblia inatueleza kuwa mbingu na nchii zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe na ndio maana wachawi awata fanya uchawi wao bila siku moja kukamatika adharani kwani atujakamata wachawi hapa? bonyeza link hii upate soma nakara hii iliyo pita kuhusu wachawi.Ninaamuru nguvu yakushinda wachawi ikufuate katika jina la Yesu ukapate kuwajua wa baya wako wote na uwajuapo tu usiwape nafasi kazi yako ni moja wewe tangaza nuru uone jinsi ambavyo mambo yako yataenda sawa.Ninapomalizia ninapenda kukushauri mwaka huu usipoteze muda kujadiri mambo yasio faa bari kaa chini kujadiri mambo yatakayo kuletea faida na sii hasara ubalikiwe sana!



Post a Comment

 
Copyright © 2015 Nabii Jiographia

Designed by Luzmik Technologies